Matukio

Habari

​DART yaanzisha Kamati ya kupokea na kushughulikia malalamiko ya fidia.

​DART yaanzisha Kamati ya kupokea na kushughulikia malalamiko ya fidia.

Martha Komba

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umeanzisha Kamati ya kupokea na kushughulikia malalamiko kupitia mafunzo yake yenye lengo la kuwaelimisha wananchi wakati, kabla ya baada ya kulipwa fidia kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa awamu ya pili ya miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka.

Mafunzo hayo yameanza kufanyika Mei 21, 2018 katika Ofisi ya Kata ya Mianzini na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka DART kwa kushirikiana na Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu kutoka Wakala wa Barabara Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Mthamini Mkuu wa DART Bw. Mouston Mwakyoma alisema kuwa wananchi wamekuwa wakisubiri kwa hamu kulipwa fidia zao ili waweze kuhama na kupisha ujenzi huo wa awamu ya pili na kwamba ni kawaida kabla,wakati na baada ya kulipa fidia kunakuwa na malalamiko mbalimbali, hivyo Serikali kupitia Wakala wake DART imeunda Kamati hiyo ili kusaidia kutatua changamoto zitakazojitokeza wakati wa fidia.

“Tunajua kwa muda mrefu mmekuwa mkisubiri kulipwa fidia zenu ili kupisha ujenzi wa awamu ya pili ya miundo mbinu ya Mabasi Yaendayo Haraka. Serikali ipo pamoja nanyi na tunawahakikishieni kuwa haitapita miezi miwili bila kulipwa fidia hiyo kwani tupo katika hatua za mwisho za uhakiki tukishirikiana na Wizara ya Fedha,” alisema Bw. Mwakyoma.

Mafunzo hayo ya kuunda Kamati ya kupokea na kushughulikia malalamiko ya fidia yataendelea kutolewa kwa muda wa wiki moja na kila itakapotikana na nafasi Maafisa Ustawi wa jamii wataendelea kuelimisha viongozi walioteuliwa kushughulikia malalamiko hayo ili wawe na uelewa wa kutosha utakaowasaidia pia kuelimisha wananchi juu ya kujaza, kuandika na kuwasilisha Malalamiko hayo.

-Mwisho-

Ramani

    Hakuna Taarifa kwa sasa