Matukio

Habari

Bodaboda zadai kujumuishwa kwenye miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka

Bodaboda zadai kujumuishwa kwenye miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ukiwa unakaribia miaka miwili sasa katika kuendesha mabasi chini ya mtoa huduma wa mpito mwezi Mei mwaka huu, Chama cha Madereva wa Pikipiki na Bajaji cha Maendeleo Tanzania (MAPIMATA), hivi karibuni kimedai njia maalum kwenye miundombinu ya DART ili kurahisisha shughuli zao.

Madai hayo ya viongozi wa bodaboda kupewa haki ya kujumuishwa kwenye mfumo wa DART umeibuka baada ya kukamatwa mara kwa mara na polisi pale wanapokiuka sheria za barabarani.

Moja ya kosa linaloangukia kwenye mfumo wa DART unaopelekea kukamatwa na polisi ni kuendesha kwenye barabara za Mabasi Yaendayo Haraka, zikiingilia njia za baiskeli na za wapiti kwa miguu.

Pia mbali na kudai njia maalum, viongozi wa chama hicho walidai kupewa sehemu maalum ya kuwashushia abiria wao badala ya kuwashusha popote wanapoona pako sawa, suala linalopelekea kutokuelewana na usumbufu kwa mamlaka za serikali na watumiaji wa miundombinu ya DART.

Mwenyekiti wa MAPIMATA, Bw. Edward Mwenisongole said, “tangu makundi mengine ya watumiaji wa Njia za Mabasi Yaendayo Haraka wamepewa nafasi ya kunufaisha mfumo, tungeshukuru kama waundaji wa njia za mabasi yaendayo haraka wangetupa njia maalum ili kuweza kurahisisha biashara zetu”. Kwa sasa tunakumbana na misongamano tele kuwabeba abiria wetu.

Ingawa bodaboda na bajaji wamejumuishwa kwenye njia ya mchanganyiko wanasema kuwa kutumia njia mchanganyiko inawafanya wasiweze kuendesha shughuli zao za kuendesha abiria kutokana na njia hizo kuwa na msongamano wa magari tofauti, hivyo kujihatarisha na ajali mbaya.

Kamanda wa MAPIMATA, Bwn. Ramadhani Ndege alitoa maoni kwamba kituo kimoja cha bodaboda kingejengwa kwenye kituo kikuu cha Kimara ili watoe huduma ya usafiri kwa watu wanaoshuka Kimara kutoka kwenye vituo vya DART.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa MAPIMATA Kanda ya Kinondoni, Bwn. Boniface Mugasi alikiri ukosefu wa elimu juu ya utumiaji wa miundombinu ya DART akisema kuwa walifikiri njia za pembeni ziliwajumuisha pia bodaboda.

Akiwajibu viongozi wa MAPIMATA, Mtendaji Mkuu wa DART, Mhandisi Ronald Lwakatare, alielezea muundo wa miundombinu ya DART na uwiano kwa watumiaji wake.

Mhandisi Lwakatare aliwaahidi viongozi hao kuwa mapendekezo yao yatapelekwa kwa mamlaka tofauti ya serikali na waundaji wa miundombinu kwaajili ya majadiliano na labda kwaajili ya utekelezaji katika awamu zijazo za mradi wa DART.

Ramani

    Hakuna Taarifa kwa sasa