Matukio

Habari

TANZIA

TANZIA

MAREHEMU BW. VICTOR NDONNE ALIYEKUWA KAIMU MKURUGENZI WA IDARA YA MAENDELEO NA USAFIRISHAJI - DART

Uongozi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) unasikitika kutangaza kifo cha ghafla cha aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Maendeleo na Usafirishaji Bw. Victor Ndonne kilichotokea jana asubuhi tarehe 1/1/2019 majira ya saa 4:00 asubuhi nyumbani kwake Yombo Vituka jijini Dar es Salaam. Msiba upo nyumbani kwa marehemu Yombo Vituka karibu na Shule ya Msingi Yombo Vituka. Taratibu za mazishi zinaendelea kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu. Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa na kusafirishwa siku ya Alhamisi tarehe 3/1/2019 nyumbani kwake na mazishi yatafanyika siku ya Ijumaa tarehe 4/1/2019 kijijini kwake Mafinga.

Uongozi unawaomba watumishi wote kushirikiana katika kipindi hiki cha msiba kwa kwenda kuwafariji wafiwa nyumbani kwa marehemu.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi na ratiba kamili ya mazishi.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA,

JINA LA BWANA LIBARIKIWE.

Ramani

    Hakuna Taarifa kwa sasa