Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
MFUMO WA DART AWAMU YA TANO
Wataalam washauri kampuni ya M/s Kunhwa toka nchini Korea wakishirikiana na kampuni ya AQGOLA kutoka Tanzania wanasimamia utekelezaji wa ujenzi wa Awamu ya Tano ya Mradi wa DART. Kampuni hizi zilipatikana kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ili kutekeleza usanifu wa kina wa miundombinu ya hii, kazi ambayo ilianza tangu katikati ya mwaka 2018. Mtaalamu Mshauri tayari amewasilisha ripoti za mwisho za usanifu wa kina na yameshajumuishwa. Serikali ya Tanzania imepata ufadhili wa mkopo kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa DART Awamu ya Tano kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) mwezi Februari 2022. Ufadhili huo unatoa kibali cha kumpata Mkandarasi wa ujenzi amabye ataanza kazi mara tu usanifu utakapokamilika. Kwa hivi sasa taratibu za RAP zinakamilishwa kabla ya zabuni ya ujenzi kutangazwa.