Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
MFUMO WA DART AWAMU YA TATU
Awamu ya tatu ya mradi inaanzia katikati ya Jiji la Dar es Salaam na inajumuisha mitaa ya Azikiwe na Maktaba, barabara za Bibi Titi na Nyerere kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) hadi eneo la Gongo la Mboto. Tawi lingine la awamu ya 3 linaanza kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Kariakoo Gerezani kupitia mitaa ya Lindi, Shaurimoyo na Uhuru hadi Buguruni inapoungana na barabara ya Nelson Mandela na kujiunga na barabara ya Nyerere kwenye makutano ya TAZARA ikiwa na urefu wa kilomita 23.6 ikiunganishwa na Awamu ya Kwanza na ya Pili ya mradi katika Vituo Vikuu vya Mabasi vya Kariakoo - Gerezani na Kivukoni. Katika awamu ya tatu ujenzi unajumuisha barabara pekee za Mabasi (exclussive BRT lanes) , barabara za magari binafsi, njia za waenda kwa miguu pamoja na baiskeli zenye jumla ya urefu wa kilomita 23.6; Vituo Vikuu vya Mabasi vitatu (3); Vituo vidogo vya Mabasi thelathini na mbili (32), karakana moja (1) ya Mabasi pamoja na Vituo mlishi vitatu (3). Ujenzi wa miundombinu ya awamu ya tatu ya Mradi wa DART unatekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Hali ya Usafiri katika Jiji la Dar es Salaam (DUTIP)