Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Deusdelity Casmir photo
Deusdelity Casmir

Mkurugenzi wa Fedha na Uhasibu

Wasifu

Ndugu Casmir, Deusdelity ni mtumishi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka akishika wadhifa wa Mkurugenzi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara tangu 2021. Ndugu Casmir yupo mahsusi kuhakikisha maendeleo endelevu ya ukuzaji wa Uchumi wa Wakala.

Ndugu Casmir kitaaluma ni msajiliwa wa bodi ya wahasibu, ni mtaaluma mwenye shahada ya uzamili ya sayansi ya Uchumi kutoka chuo cha Strathclyde nchini Uingereza akibobea katika portfolio management, analysis ya usalama,manejiment ya hazina na project financing na Evaluation. Pia ana Advanced Diploma katika Accountancy ya chuo kikuu cha usimamizi wa fedha kilichopo jijini  Dar es salaam nchini Tanzania(IFM)

Ndugu Casmir ana uzoefu wa miaka 20 katika fani ya uhasibu akihudumu katika ngazi ya manejimenti kwenye sekta ya umma na binafsi zikiwemo taasisi za kimataifa. Ndugu Casmir alianzia safari yake ya kiutumishi wa umma katika Shirika la simu Tanzania (TTCL) alipohudumu kwa miaka mitano kama mhasibu. Baada alipandishwa cheo kuwa mhasibu wa kanda kabla ya kuhama shirika 2004 kwenda  kuwa mhasibu wa programu ya sekta ya kilimo chini ya Ubalozi wa Denmark. Pia alihudumu kama Mhasibu mkuu wa Mamlaka ya maendeleo ya biashara nchini Tanzania. Anahuduma kama mkurugenzi mtendaji wa kujitegemea katika kampuni ya Taasisi ya Tekinolojia Dar es salaam na pia ni Mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango wa bodi. Vilevile ni mwenyekiti wa kamati ya ukaguzi ya wakala wa usajili wa vizazi na vifo Tanzania. Ndugu Casmir anauzoefu wa kina katika usimamizi wa fedha, biashara za kimataifa, Usimamizi wa kodi na Uwekezaji.