Tiketi ya Msimbokodi
Tiketi ya Msimbokodi
Hii ni tiketi ya karatasi yenye Msimbokodi.
NI WAPI NAWEZA KUINUNUA?
Unaweza kununua tiketi yenye Msimbokodi katika kituo chochote cha Mabasi Yaendayo Haraka.
ITATUMIKA KWA MUDA GANI?
Tiketi ya Msimbokodi inaweza kutumika ndani ya dakika 30 tangu kununuliwa kwake.
JE, NAWEZA KUNUNUA TIKETI YA MSIMBOKODI ENEO LOLOTE?
Hapana, tiketi ya Msimbokodi itatumika katika kituo ulichonunulia tu.
NI MAMBO GANI YANAANGALIWA WAKATI WA KUHAKIKI TIKETI YA MSIMBOKODI?
Mambo matatu yanaangaliwa wakati wa kuhakiki tiketi ya Msimbokodi.
- Uhalali wa tiketi
- Muda sahihi wa matumizi ya tiketi husika
- Kituo sahihi cha kupandia basi
- Endapo imedurufiwa