Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

"

Kwa kushirikiana na Wakala wa ujenzi wa Barabara Tanzania (TANROADS), Wakala wa DART umekuwa ukiondoa uchafu na mchanga katika mto Msimbazi na eneo la Jangwani kama mkakati wa muda mfupi ili kurahisisha upitaji wa maji. Zaidi ya hivyo, kuna mpango wa muda mrefu unaofanywa na Mradi wa DMDP(Dar es Salaam Metropolitan Development Programme) chini ya TAMISEMI na Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam. Mradi huu uko chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia ili kutafuta ufumbuzi wa yanayolikumba bonde la Msimbazi hususani mafuriko. Mpaka sasa mradi huo umemshirikisha mtaalamu ambaye anafanya usanifu wa kuonesha kinachotakiwa kufanyika ili Jangwani na bonde zima la Msimbazi lisikumbwe na majanga ya mafuriko. 

"

"

Kwanza hii ni huduma ya mpito ambapo ilikuwa itekelezwe kwa muda wa miaka miwili, katika kipindi hicho mtoa huduma alipewa nafasi ya kuingiza Mabasi. Mabasi hayo yamegawanywa katika njia saba kwenye njia kuu na njia tano kwenye njia za mlisho. Ili kutoa huduma kamili, mpango ulikuwa mabasi yaletwe 305 kwa ajili ya kutoa huduma katika njia saba za njia kuu na njia mbili. Kufikia lengo hilo, Wakala upo katika mchakato wa kumpata mtoa huduma atakayetoa huduma kamili.

Lengo kuu la kuanzisha mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka-BRT ni kuwashawishi watu kutumia Mabasi makubwa yenye kuchukua abiria wengi kwa wakati mmoja ili kupunguza ili kupunguza kishawishi cha watu kutumia magari yao binafsi na hivyo kuepuka mfumo wa zamani wa usafiri wa umma ambao unatumia mabasi yenye ujazo mdogo unaowafanya watu wengi kushindwa kufika mapema wanakokwenda na hivyo kusababisha watu wengi wapende kuendesha magari barabarani. Hivyo, isingekuwa jambo la busara kuruhusu tena mfumo wa zamani ushamiri. Ili kuondoa changamoto katika kutoa huduma ya Mabasi katika mfumo wa DART ni kwa Wakala kuharakisha taratibu za manunuzi za kumpata mtoa huduma kamili ambaye pia ataongeza idadi ya Mabasi katika mfumo kutoka 140 hadi kufikia 305 katika Awamu ya Kwanza.

"

"

Kwa kawaida, mtoa huduma huweka mabasi barabarani wakati abiria wakiwa wengi (peak hours) na mabasi asilimia 75 wakati abiria wakiwa wachache (off peak).Hapo awali, kabla ya karakana ya Jangwani kukumbwa na mafuriko mabasi yalikuwa yanaenda kuegeshwa kwenye karakana ya Jangwani wakati abiria wakiwa wengi(peak hour) na baadhi ya mabasi kuegeshwa wakati abiria wakiwa wachache (off peak). Ila kipindi ambacho mafuriko yalitokea Mabasi yalikuwa yanaegeshwa maeneo tofauti hasa katika vituo vikubwa. Pia, madereva huwa wanaegesha mabasi kwa kuzingatia ratiba maalum ya Mabasi ambayo imeandaliwa na wataalam kwa kuzingatia mahitaji ya usafiri katika njia husika. Hivyo, sio sahihi kuwa Mabasi yanaegeshwa tu bila utaratibu rasmi. 

"

"

Changamoto ya kuchelewa kwa mabasi inatokana na na kutokukamilika  kwa mfumo wa kufuatilia mwenendo wa magari  katika mfumo(Intelligent Transportation System - ITS unaowezesha maafisa walioko kwenye kituo cha usimamizi wa mwenendo wa mabasi (Control Centre) kujua ni sehemu zipi katika mfumo zinahitaji idadi kubwa au ndogo ya mabasi kwa muda husika. Mfumo wa ITS ukikamilika kusimikwa katika mfumo wa DART tatizo la kuchelewa kwa mabasi kufika vituoni litapungua kwa kiasi kikubwa. Kwenye kipindi cha mpito, kuna jumla ya Mabasi 120 badala ya kuwa na mabasi 305 kama mtoa huduma kamili ya mabasi angekuwa amepatikana. Upungufu wa mabasi kwa baadhi ya siku unatokana na matengenezo ya kawaida unaosababisha wakati mwingine kuwa na uhaba wa mabasi na hivyo kuwa na msongamano kwenye vituo. Wakala uko katika hatua za manunuzi  ya kimataifa za kumpata mtoa huduma kamili kwenye mfumo ambaye pia  ataongeza idadi ya mabasi kwa kufuata sheria na taratibu za manunuzi za Serikali. Hata hivyo, Wakala wa DART unashirikiana kwa karibu na mtoa huduma ya mpito ili kuhakikisha huduma ya Mabasi inaboreshwa licha ya changamoto zilizopo. 

"

"

DART imepata hasara mbalimbali ikiwemo abiria wake kukosa huduma kwa wakati kutokana na ubovu wa baadhi ya mabasi uliotokana na mafuriko ya Jangwani, Pia hasara ya kugharamia urekebishaji wa mabasi yaliyoharibika, kusafisha karakana, mitaro na barabara wakati wa mafuriko. Hasara nyingine ni kushuka kwa mapato ya kila siku kutokana na uchache wa mabasi.

"

"

Maamuzi ya kujenga karakana Jangwani yalifanyika baada ya kufanya tathmini ya athari za mazingira (Environmental Impact Assessment)na kubaini kuwa eneo hilo lingefaa. Hata hivyo, kwa siku za karibuni kumekuwa na uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu katika maeneo  ya  juu ya bonde la Mto Msimbazi ikiwa ni pamoja na watu kujenga  na kutupa takataka ndani ya bonde la mto huo, vitu ambavyo vinabadili mwendo wa maji wakati wa mvua nyingi. 
Mchanga mwingi na takataka ni matokeo yanayosababisha maji ya mvua kushindwa kutiririka vizuri kuelekea baharini. 

 

"