Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Mwendokasi App
Mwendokasi App

Programu Tumizi ya Mwendokasi inakusaidia katika..

  • Kukata tiketi
  • Kupanga safari 
  • Kutoa taarifa ya tukio lililotokea katika ushoroba
  • Kufahamu endapo kuna changamoto imetokea ambayo inaathiri au imeathiri huduma kwamfano ajali, mafuriko nk.
  • Kuona njia za (uelekeo wa) mabasi na ratiba za mabasi husika.
  • Kupata habari na kufahamu maswali yanayoulizwa mara kwa mara.

 

Sasa unaweza kukata tiketi yenye Msimbokodi kirahisi kupitia Programu tumizi. Tiketi yenye Msimbokodi iliyonunuliwa kupitia Programu Tumizi ina sifa zifuatazo; 

  • Tiketi inakwisha muda wa matumizi baada ya saa tatu kupita.
  • Kituo unachokichagua ndicho utakachokitumia kupandia basi.
  • Hutaweza kubadilisha kituo mara baada kununua tiketi.

Sasa unaweza kununua tiketi kupitia Programu Tumizi ya Mwendokasi  

 

 

 Faida ya kutumia Program Tumizi

  • Kuepuka kusimama katika foleni ya kunua tiketi
  • Inaokoa muda
  • Huitaji kutembea na fedha
  • Unaweza kuona miamala yako

 

 

 

Inapatikana bure kwa Watumiaji wa simu zenye Mfumo wa Playstore and App Store kwa Watumiaji wa simu zenye Mfumo wa I.O.S