Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Kituo Cha Usimamizi WA Hali Ya Nyendo Za Usafiri

Zipo faida nyingi zilizothibitishwa kidunia zikihusishwa kwa taasisi kuwa na Kituo cha usimamizi wa mwenendo wa magari kama  vile ubadilishanaji wa taarifa, rasilimali na teknolojia pamoja na mwingiliano wa uendeshaji, usimamizi wa mtandao wa BRT, ufanyaji wa maamuzi pamoja, usimamizi wa matukio na kuchukua hatua stahiki wa shughuli zote za mfumo wa BRT kwa ujumla wake

Kituo cha usimamizi wa mwenendo wa magari kinahifadhi kompyuta kuu zinazohitajika kushirikiana na Mfumo nadhifu wa kuongozea magari ili kukidhi ufanyaji kazi ya usimamizi. Kituo cha udhibiti kinajumuisha mfumo wa ufuatiliaji kupitia video kwa waendeshaji zinazopokea picha za kamera eneo la tukio.

Kituo cha udhibiti vilevile kinahusisha wadau muhimu kama vile wahandisi idara ya taa za kuongozea magari, polisi pamoja na wataalam kutoka idara ya huduma za dharura.

Katika Kituo cha Udhibiti, taarifa hukusanywa kutoka ndani ya mabasi kisha kupelekwa kwenye kituo cha udhibiti zinakochakatwa. Kutoka kituo cha udhibiti, taarifa muhimu, zilizopo katika aina ya GTFS na GTFS-RT, hutumwa kwenye Web Display Feed (WDF), Onyesho za Habari za Umma (PID) kwenye vituo. Wafanyikazi katika Kituo cha Uendeshaji wa Usafiri pia wanawajibika kuwasiliana na maafisa waliopo vituoni mfano madereva, wafanyikazi wa usalama na wahudumu wa kituo.