Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Eliphas Mollel photo
Dkt. Eliphas Mollel

Mkurugenzi wa Kitengo cha Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala

Wasifu

Dkt. Eliphas Mollel ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala mwenye dhamana ya kusimaimia mikakati ya kimaendeleo, na usimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya rasilimali watu na utawala.

Sifa

Dkt. Mollel ana shahada ya rasilimali watu na utawala akibobea katika masuala ya uwajibikaji na usimamizi wa fidia kutoka Chuo Kikuu cha Moi nchini Kenya. Dkt. Mollel ana shahada ya uzamili katika Uongozi wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Coventry nchini Uingereza. Pia ana Shahada ya Uzamili ya Utawala akibobea katika usimamizi wa rasilimali watu kutoka Chuo Kikuu cha Botswana. Dkt. Mollel ana Shahada ya Utawala akibobea katika usimaizi wa rasilimali kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro Tanzania.

Uzoefu wa Kazi

Dk. Mollel ana uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika usimamizi wa rasilimali watu  na utawala kwenye Sekta ya Umma na Binafsi ya Tanzania. Amefanikiwa kufanya kazi mbalimbali za kubuni, kufanya mapitio na utekelezaji wa sera za rasilimali watu katika sekta ya umma na binafsi Tanzania. Dkt. Mollel amekuwa Mkuu wa Rasilimali Watu na Utawala katika Halmashauri mbalimbali pamoja na Benki ya Biashara. Vilevile Dkt. Mollel ni Mhariri katika Bodi mbili za Kimataifa za majarida ya utafiti katika masuala ya Elimu na Jarida la Africa Mashairiki la Elimu na Sayansi ya Jamii. Pia anahudumu kama mjube wa bodi  na mwenyekiti wa bodi katika taasisi mbili.