Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Mohamed Kuganda photo
Mhandisi Mohamed Kuganda

Kaimu Mkurugenzi

Wasifu

Mha. Mohamed Kuganda ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji aliyekabidhiwa jukumu la kupanga, kusanifu na kujenga miundombinu ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART). Amekuwa mtumishi wa Serikali kwa miaka 22 ambapo kwenye DART ametumikia kwa zaidi ya miaka 18.

Elimu

Mha. Kuganda ni Mhandisi Ujenzi kitaaluma aliyebobea kwenye usafirishaji (transportation). Amesajiliwa na Bodi ya Usajili ya Wahandisi Tanzania (ERB). Amepata shahada ya Sayansi ya Uhandisi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Tanzania, Stashahada ya Usalama barabarani katika Chuo Kikuu cha Lund (Sweden), Stashahada ya Mpango, uendelezaji na usimamizi wa usafiri wa umma mijini katika Chuo cha Kimataifa cha Galilee - Israel pia ana cheti cha kitaaluma kwenye sekta ya mipangomiji na usafiri wa Umma kilichotolea na JICA Tokyo International Centre - Japan. Vilevile Mha. Kuganda ana cheti cha kitaaluma kwenye masuala ya miradi ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, hatua ya Msingi, Certified PPP Professional – Foundation level.

Uzoefu

Mha. Kuganda amefanya kazi za usanifu wa mradi wa DART mwaka 2005 na kufanikisha kuandaliwa kwa Mpango Kabambe wa utekelezaji wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka ambao ulipangwa kutekelezwa kwa awamu 6 kwenye barabara kuu za usafiri wa umma jijini Dar es Salaam. Aidha kwa mwaka 2006 hadi 2007 amekuwa mjumbe wa timu maalum ya uanzishwaji wa Wakala wa DART kwa ajili ya kujenga miundombinu na kusimamia usafiri wa umma Dar es Salaam unaotumia mabasi makubwa (DART system). Mwaka 2008 amekuwa mjumbe wa timu ya wataalamu walioshiriki kuandaa Mpango Kabambe wa Usafiri wa Umma jijini Dar es Salaam (DUTMP) kwa kushirikiana na timu ya wataalamu kutoka JICA.

Akihudumu katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Wakala wa DART, Mha. Kuganda amesimamia kazi za kupanga, kusanifu (wa awali) na usanifu wa kina kwa awamu ya 2, 3, 4 na 5 ya mradi wa DART. Aidha Mha. Kuganda ni mratibu wa mradi wa maboresho kwenye ushoroba wa DART yaani Transit Oriented Development (TOD), lengo la mradi ni kuwa na usafiri endelevu wa umma katika miji.