Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
FLORA FIFI photo
CPA. FLORA FIFI

Head of Internal Audit Unit

Wasifu

CPA. Flora Naftal Fifi ni Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani mwenye dhamana ya kusimamia kikamilifu shughuli za ukaguzi wa ndani kwa mujibu wa Miongozo  mbalimbali ya Ukaguzi wa Ndani na uhakiki wa mifumo kulingana na udhibiti wa vihatarishi; kuandaa taarifa za ukaguzi wa ndani na kuwasilisha kwa Mtendaji Mkuu na Kamati ya Ukaguzi ; kufanya ukaguzi maalum; kufuatilia utekelezaji wa ushauri wa taarifa za ukaguzi; kuandaa mpango kazi wa mwaka wa ukaguzi wa ndani pamoja na kushauri kuhusu matumizi bora ya rasilimali za  Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).


Sifa
CPA. Flora ana Stashahada ya Uzamili ya Uhasibu na Stashahada ya Juu ya Uhasibu zote  kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha Tanzania. Amethibitishwa na Bodi ya Kitaifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kuwa Mhasibu wa Umma (CPA).

Uzoefu wa Kazi
CPA Flora ana uzoefu mkubwa katika Ukaguzi, utawala wa kitaasisi, mkakati, majanga, na usimamizi wa fedha. Kabla ya kujiunga na DART, CPA. Flora alikuwa Mkaguzi Mkuu Msaidizi kwa miaka 8 akifanya kazi na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa zaidi ya miaka 30.