CPA. Wakili Jerome Pantaleo Rweshagara
Mkurugenzi wa Biashara na Uwekezaji
Wasifu
CPA. Wakili Jerome Pantaleo Rweshagara ni Mkurugenzi wa Biashara na Uwekezaji, Mwenye dhamana ya kusimamia Shughuli za Masoko,Huduma kwa Wateja na Uwekezaji ,ili kuiwezesha Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka(DART) kujiendesha kibiashara na kujitegemea huku ikitoa huduma bora kwa wadau mbalimbali .
CPA. Wakili Jerome Pantaleo Rweshagara ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 akibobea kwenye Uendeshaji wa Biashara ,Manunuzi ,Uhasibu na Sheria.Vilevile,Ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama zilizo chini yake ,ni Mjumbe wa Bodi ya Rufani za Kodi TRAB) ,amesajiliwa na Bodi Mbalimbali za Kitaaluma ikiwemo Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu(NBAA) na Bodi ya Manunuzi na Ugavi(PSPTB). Vilevile ni Arbitrator katika Baraza la Taifa la Ujenzi(NCC) ,na Tanzania Arbitration Centre, iliyopo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria.
CPA. Wakili Jerome Pantaleo Rweshagara ana Shahada ya Uzamili katika Uendeshaji Biashara(MBA) kutoka Chuo Kikuu Mzumbe,Stashahada ya Juu ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo kutoka Law School of Tanzania(LST) ,CPA(T) kutoka Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu(NBAA),CSP(T) kutoka Bodi ya Ununuzi na Ugavi(PSPTB) na Shahada ya Kwanza ya Sheria (LL.B).