Dkt Zanifa Omary Limboa
Mkurugenzi wa Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
Wasifu
Dkt. Zanifa Omary Limboa ni Mkurugenzi wa TEHAMA mwenye dhamana ya kusimamia mifumo na miundombinu ya TEHAMA ikiwemo Usanifu, Upatikanaji wa vifaa, programu na mtandao wa mawasiliano ya TEHAMA ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka na katika Mfumo wa DART. Dkt. Zanifa Omary Limboa ana uzoefu wa zaidi ya miaka 17 akibobea kwenye Sayansi ya Kompyuta.
Dkt. Zanifa ana Shahada ya Uzamivu katika Sayansi ya Kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia Dublin (Technological University Dublin), Jamhuri ya Ireland. Pia ana Shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia Dublin (Technological University Dublin), Jamhuri ya Ireland na Diploma ya Juu ya Sayansi ya Kompyuta kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).