DART yafanya mafunzo kwa Watoa huduma Mradi wa DART Mbagala
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka – DART leo October 24, 2025 umeanza mafunzo kwa maafisa wanaohudumu kwenye Mradi wa DART Awamu ya Pili inayoelekea Mbagala.
Akiongea wakati wa mafunzo hayo Kaimu Meneja wa Oparesheni DART, Mhandisi Joseph Lubilo amesema lengo la mafunzo ni hayo ni kuwakumbusha maafisa hao majukumu wanayotakiwa kuyatekeleza ili wakahudumie vyema abiria wa mabasi Yaendayo Haraka.
“Kama mnavyofahamu tumeanza mafunzo ya vijana wetu wa Mofat ambao wanatoa huduma katika mabasi ya Mofat, mabasi hay ani mapya na hii njia ya Phase two ni mpya na waajiriwa hawa ni wapya kwa hiyo tumeona bora tukae nao tuwape majukumu wanayotakiwa kufanya hususani katika kusimamia katika utoaji wa huduma kwa abiria ipasavyo na huduma nyinginezo” alisema Mhandisi Lubilo.
Mhandisi Lubilo ameongeza kuwa mara baada ya kuwapatia mafunzo hayo, DART itakuwa na jukumu la kuwatembelea na kukagua kuona kama mkataba waliosaini unafuatwa.
“Wakishafahamu majukumu yao nasi tutapata nafasi kukutana nao, kuwatembelea na kuwakagua kuona kwamba wanafanya kazi kulingana na mkataba ambao tumeingia nao.
Aidha katika mafunzo hayo, mada mbalimbali zitafundishwa ikiwemo Huduma za Wakala, Huduma kwa Wateja, Usalama wa abiria, Nidhamu kazini, Afya na usalama kazini pamoja na Kaizeni kuboresha huduma.
Mafunzo hayo yatakayoendeshwa kwa siku mbili yanahusisha Maafisa 200 kutoka kwa Mtoa Huduma ya Mabasi Kampuni ya Mofat katika kada ya Mafisa Usafirishaji, maafisa Operesheni na maafisa watoa huduma kwa abiria.
