Fahamu kuhusu Mwendokasi Kadi
Fahamu kuhusu Mwendokasi Kadi
03 Sep, 2024
- Kadi ya Mwendokasi inauzwa kwa Shilingi 5,000/= malipo halali ya fedha za Kitanzania.
- Unapaswa kuisajili Kadi ya Mwendokasi kwa kutumia Kitambulisho cha Taifa au Kitambulisho cha Kura au Leseni ya Udereva na au Hati ya Kusafiria.
- Ili uweze kuitumia Kadi ya Mwendokasi katika kulipa nauli ya huduma ya usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka mara baada ya kuinunua na kuisajili, utapaswa kuiwekea fedha.
- Utaweza kuiwekea fedha Kadi ya Mwendokasi kupitia njia mbalimbali kwa mfano kupitia Afisa Mkatisha Tiketi aliyeko Kituoni, Mitandao ya Simu, Benki au Mwendokasi App katika kipengele cha E-Wallet.
- Kiwango cha juu cha fedha inayoweza kuwekwa katika Kadi ya Mwendokasi ni shilingi 50,000/= endapo utaweka fedha kwa Afisa Mkatisha Tiketi Kituoni mwenye kifaa cha Ticket Office Machine (TOM).
- Aidha shilingi 90,000/= ni kiwango cha juu kuwekwa katika Kadi ya Mwendokasi kwa abiria atakayejihudumia mwenyewe kupitia Mitandao ya Simu na Benki.
- Abiria atakayejihudumia mwenyewe kwa kuweka fedha katika Kadi ya Mwendokasi kupitia Mitandao ya Simu au Benki, anapaswa kuhakikisha kuwa hakosei namba zilizoko katika kadi yake (control number) kwani kwa kufanya hivyo fedha zake zitakwenda kwa abiria mwingine.
- Kwa Abiria atakayezidisha kiwango cha juu cha fedha kilichoidhinishwa kuwekwa katika Kadi ya Mwendokasi, fedha zake zitahifadhiwa na hatoziona hata atakapoangalia salio hadi pale kiwango cha juu kilichoidhinishwa kianze kupungua katika matumizi anayoyafanya.
- Hata hivyo kwa sasa Abiria anapaswa kuzingatia kuwa fedha atakazoweka katika Kadi ya Mwendokasi ni kwa ajili ya kulipa nauli katika usafiri wa Mabasi yaendayo Haraka maarufu Mwendokasi na si vinginevyo.