Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Faida ya kuunganisha Kadi ya Mwendokasi na App ya Mwendokasi
19 Sep, 2024
Faida ya kuunganisha Kadi ya Mwendokasi na App ya Mwendokasi

Mfumo wa Seriklai wa Ukusanyaji Nauli katika Mabasi Yaendayo Haraka ujulikanao kama 'Automated Fare Collection System' (AFCS) umewezesha kuunganishwa kwa Kadi ya Mwendokasi na Programu Tumizi ya Mwendokasi (Mwendokasi App) ili kumrahisishia abiria kuona taarifa mbalimbali za kadi yake. Taarifa hizo ni;

 

1. Taarifa ya vituo ambavyo Abiria ulivyovitumia kuchanja Kadi yako,

2. Tarehe ambazo Abiria ulisafiri,

3. Muda au Saa, Abiria ulipoingia Kituoni

4. Kiasi cha nauli Abiria alichotozwa kwa kila safari,

5. Kuona salio lililobaki kwenye kadi yake baada ya kutozwa kiasi cha nauli kwa kila safari,

6. Vilevile Abiria utaona historia ya miamala aliyoifanya kwenye kadi yake.