Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Hatua za kuhamisha salio kutoka Mwendokasi App kwenda katika Kadi ya Mwendokasi
10 Sep, 2024
Hatua za kuhamisha salio kutoka Mwendokasi App kwenda katika Kadi ya Mwendokasi
  1. Fungua Programu Tumizi ya Mwendokasi (Mwendokasi App) katika simu janja yako.
  2. Bofya kitufe lichoandikwa ‘Kata tiketi’.
  3. Ingiza namba ya siri kuthibitisha akaunti yako.
  4. Bofya kitufe cha ‘Hamisha salio’.
  5. Chagua kitufe cha ‘Hamisha kwenda kwenye Kadi’.
  6. Andika namba ya kadi ya yule unayemuhamishia salio halafu weka kiasi kisha bonyeza kitufe cha ‘Tuma taarifa’.
  7. Hakiki taarifa ya Jina la mpokeaji, Namba ya kadi na Kiasi halafu bofya neno ‘Tuma’.
  8. Thibitisha taarifa za uhakiki wako kwa kubonyeza neno ‘Ndio’.
  9. Utapokea ujumbe kukujulisha muamala umefanikiwa.

Hivyo ndivyo utakavyoweza kuhamisha salio kutoka Mwendokasi App kwenda katika Kadi ya Mwendokasi na utapenda kujiridhisha muamala wako umefanikiwa, angalia salio katika App kwa ku ‘refresh’ au kuifunga App ya Mwendokasi na kisha kuifungua tena utaona salio lako limepungua.