Hatua za kuisajili Kadi ya Mwendokasi na App ya Mwendokasi
Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Nauli katika Mabasi Yaendayo Haraka ujulikanao kama 'Automated Fare Collection System' (AFCS) umewezesha kuunganishwa kwa Kadi ya Mwendokasi na Programu Tumizi ya Mwendokasi (Mwendokasi App) ili kumrahisishia abiria kuona taarifa mbalimbali za kadi yake. Ili uweze kuunganisha Kadi yako ya Mwendokasi na Mwendokasi App fuata hatua zifuatazo;
- Fungua Mwendokasi App kwenye Simu Janja yako,
- Bonyeza kitufe kilichoandikwa Kadi, kipo upande wa chini,
- Baada ya kufunguka bonyeza kitufe kilichoandikwa “Add Card”,
- Utaweka namba ya kadi yako. Hii inapatikana upande wa mbele wa Kadi yako ikiwa tarakimu 12,
- Utaletewa ujumbe unaokuhitaji kuingiza 'One Time Password (OTP)'. Namba hii ya OTP itatumwa kwenye simu yako,
- Baada ya kuingiza namba ya OTP, App itafunguka kwenye sehemu iliyoandikwa Kadi Zangu. Ukiwa hapo utaweza kuona kitufe cha Vituo Ulivyotumia Kadi na kitufe cha Historia ya Miamala.
Aidha kupitia vitufe hivyo Abiria ataona taarifa mbalimbali za Kadi yake kama vile Taarifa ya vituo alivyovitumia kuchanja Kadi yake, Tarehe alizosafiri, Muda au Saa alipoingia Kituoni, Kiasi cha nauli alichotozwa kwa kila safari, Kuona salio lililobaki kwenye kadi yake baada ya kutozwa kiasi cha nauli kwa kila safari na Vilevile kuona historia ya miamala aliyoifanya kwenye kadi yake.