Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Jinsi ya kuweka salio kwenye Kadi ya Mwendokasi kupitia Mitandao ya Simu
11 Sep, 2024
Jinsi ya kuweka salio kwenye Kadi ya Mwendokasi kupitia Mitandao ya Simu

Halotel

  • Piga *150*88#
  • Chagua 4 Lipa bili
  • Chagua 5 Malipo ya Serikali
  • Ingiza kumbukumbu namba
  • Ingiza Kiasi
  • Ingiza Pin
  • Bonyeza 1 kuthibitisha
  • Utapokea ujumbe utakaokujulisha malipo ya muamala yanafanyiwa kazi.

 

Vodacom

  • Piga *150*00#
  • Chagua 4 Lipa kwa M-Pesa
  • Chagua 5 Malipo ya Serikali
  • Chagua 1 weka namba ya kumbukumbu
  • Weka namba ya malipo
  • Weka kiasi
  • Weka namba ya Siri kukamilisha malipo
  • Bonyeza 1 kufanya malipo ya AFCS
  • Utapokea ujumbe kukujulisha ombi lako linashughulikiwa.

 

Tigo

  • Piga *150*01#
  • Chagua 4 Lipa Bili
  • Chagua 5 Malipo ya Serikali
  • Chagua 1 ingiza namba ya malipo
  • Weka kiasi
  • Chagua 2 ingiza kiasi
  • Weka namba ya siri kuthibitisha
  • Utapokea ujumbe unaokujulisha malipo yamekamilika

 

Airtel

  • Piga*150*60#
  • Chagua 5 Lipa Bill
  • Chagua 5 Malipo ya Serikali
  • Chagua 1 Ingiza control number
  • Ingiza kiasi cha pesa
  • Weka namba ya Siri kulipia
  • Utapokea ujumbe utakaokujulisha ombi lako linashughulikiwa.

 

Ttcl

  • Piga *150*71#
  • Chagua 4 Lipa bili
  • Chagua 6 Malipo ya Serikali
  • Weka namba ya kumbukumbu
  • Weka kiasi
  • Ingiza namba ya siri kuthibitisha malipo
  • Utapokea ujumbe unaokujulisha malipo yamepokelewa