Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Mfumo nadhifu wa kuongezea magari kukamilika miezi sita ijayo
26 Oct, 2023
Mfumo nadhifu wa kuongezea magari kukamilika miezi sita ijayo

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) imeihimiza kampuni ya IDOM ya nchini Hispania kukamilisha kazi ya kusanifu na kusimika mfumo nadhifu wa kuongoza magari - ITS ifikapo Juni 2024.

 

Hayo yamebainishwa Oktoba 26, 2023 na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dr. Edwin Mhede wakati wa Mkutano wa Kitaasisi wa uzinduzi wa utekelezaji wa Mfumo ITS kwenye Mfumo wa DART.

 

Katika mkutano huo ulioshirikisha taasisi wadau, Dr. Mhede amesisitiza kuwasimamia kikamilifu wataalam washauri kutoka kampuni ya IDOM inatakayohusika kusanifu na kusimika mfumo wa huo.

 

“Kwenye muendelezo wa safari yetu ndefu iliyoanza hata kabla ya uhuru ya kuboresha usafiri wa umma mijini, leo tunafikia kwenye kitu ambacho si zaidi ya miezi sita ijayo tutakuwa na mfumo nadhifu wa kuongozea mabasi” Alisema Dr. Mhede

 

Pia Dr. Mhede amewaomba wananchi kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki ambapo wakala unapambana kuhakikisha huduma inakuwa bora zaidi kwa ajili ya shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

 

Akichangia katika mkutano huo, Kamanda wa Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam Murilo Jumanne amesema mbali na suala la kiusalama ITS itasaidia kuondoa askari wa kuongoza magari katika makutano na badala yake askari hao watatumika katika majukumu mengine ya kulinda usalama wa raia na mali zao.

 

Naye Balozi wa Hispania nchini Tanzania Bw. Jorge Moragas aliyeshiriki uzinduzi huo ameiahidi ushirikiano wa dhati kuhakikisha kampuni ya IDOM inatekeleza kazi hiyo kwa ukamilifu kama ilivyokusudiwa ili kufungua milango kwa taasisi nyingine kutoka nchini kwake kuja kuwekeza nchini.

 

Mfumo wa ITS ukikamilika utasaidia kuondoa changamoto ya uchelewaji wa magari kwenye makutano ya barabara za mabasi Yaendayo Haraka na magari mengine.

 

Mbali na kuongozea magari, pia utasaidia kufahamu idadi ya mabasi yanayohitajika na usalama wa abiria na zao wakiwa kwenye safari ndani ya Mfumo wa DART.

 

Taasisi wadau wanahusika katika utekelezaji wa mfumo wa ITS ni LATRA, TANROADS, JESHI LA POLISI, TARURA, TEMESA, UDART, eGA, TCRA, UDART, Wizara ya Fedha, Wizara ya Uchukuzi,Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na JICA na Benki ya Dunia.