Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Mfumo wa DART Awamu ya Sita

Awamu ya Sita ya mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka itahusisha barabara za Mwai Kibaki, na barabara za nyongeza (extension) ya Awamu ya Kwanza kutoka Kimara Mwisho hadi Kibaha na nyongeza (extension) ya Awamu ya Pili kutoka Mbagala Rangi Tatu hadi Vikindu zenye urefu wa kilometa 33.5.

 

Kwa sasa Wakala unaendelea na hatua za kutafuta fedha kwa ajili ya usanifu wa kina na ujenzi wa miundombinu, ambapo tayari Wakala kwa kushirikiana na CRDB Bank PLC, wamewasilisha andiko Secretariati ya Green Climate Fund (GCF), ili kuomba ufadhili wa fedha za kutekeleza mradi huo.