MFUMO WA DART AWAMU YA TANO
MFUMO WA DART AWAMU YA TANO
Awamu ya Tano ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka itahusisha barabara za Nelson Mandela, barabara ya Mbagala na barabara ya Tabata -Segerea – Kigogo zikiwa na jumla ya urefu wa kilometa 26.0. Usanifu wa kina ulifanywa na kampuni ya Kunhwa Engineering & Consulting Co. Ltd ya Korea Kusini.
Aidha, Serikali ya Ufaransa kupitia taasisi yake ya AFD (French Development Agency) imetoa mkopo wa fedha kugharamia ujenzi wa miundombinu ya Awamu hiyo ya Tano. Tayari Mhandisi mshauri wa ujenzi amepatikana, na kwasasa TANROADS akishirikiana na Wakala wametangaza zabuni kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi.