Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
MFUMO WA DART AWAMU YA NNE
Awamu ya nne inaanzia katikati ya Jiji kwenda Tegeta (Boko Basihaya), ikijumuisha barabara za Bibi Titi, Ali hassan Mwinyi na Bagamoyo, pia ina tawi linaloanzia Mwenge hadi Ubungo kupitia barabara ya Sam Nujoma ikiwa na jumla kilomita 30.1. Ujenzi unatekelezwa kwa mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia kupitia mradi wa Uboreshaji wa Hali ya Usafiri katika Jiji la Dar es Salaam (DUTP). Usanifu wa kina (Detailed Engineering design) wa mradi huu ulifanywa na kampuni ya Kunhwa Engineering & Consulting Co., LTD ya Korea Kusini kwa kushirikiana na kampuni ya AQGOLA Engineering & Management Services LTD ya Tanzania. Tayari Wakandarasi wa ujenzi wamepatikana na mikataba ya ujenzi imesainiwa tangu tarehe 30 Juni 2023 na ujenzi unaendelea kwa kasi kubwa. Aidha, kazi za ujenzi katika awamu ya Nne zinahusisha pia upanuzi wa daraja la Salender, ujenzi wa Vituo Vikuu 2, Vituo vya Mabasi 20, na Vituo Mlishi 10. Ujenzi unatekelezwa na Mkandarasi Kampuni ya China Geo-Engineering Corporation kutoka China.