Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
MFUMO WA DART AWAMU YA PILI
Awamu ya pili ya mradi inajumuisha barabara za Kilwa (kutoka katikati ya Jiji hadi eneo la Mbagala Rangitatu), Sokoine Avenue (kutoka mtaa wa Zanaki hadi mzunguko wa Gerezani), mtaa wa Gerezani (kutoka mzunguko wa Gerezani hadi Kamata kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na Msimbazi), mtaa wa Bandari (kutoka mzunguko wa Gerezani hadi Bendera tatu), barabara ya Chang'ombe (kutoka mzunguko wa Jitegemee hadi VETA kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na Kawawa) na barabara ya Kawawa Kusini (kutoka VETA kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na Chang'ombe hadi Magomeni kwenye makutano ya barabara za Kawawa na Morogoro) ikiwa na jumla ya kilomita 20.3. Ujenzi wa barabara katika Awamu hii ulianza rasmi mwezi Mei, 2019 ambapo hadi Juni 2024 ujenzi ulikua umefikia asilimia 99 zikiwa zimebakia kazi ndogo za kufunga taa za kuongozea magari (traffic lights). Awamu hiyo pia ilijumuisha ujenzi wa majengo ikiwa ni ujenzi wa karakana, ujenzi wa Vituo vikuu vya Mabasi, pamoja na ujenzi wa Vituo mlishi .Kazi hizo za ujenzi ambazo zilianza 1 Machi 2019 zimekamilika kwa kwa asilimia 100, na tayari miradi hiyo imekabidhiwa kwa Wakala.