Taarifa kwa Umma kuhusu utapeli wa kimtandao
TAARIFA KWA UMMA
YAH: Utapeli wa kimtandao
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART, unapenda kuwataarifu wateja wake na umma kuwa kuna watu wanaosambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii hasa kwa wahitimu wa vyuo vikuu wakiwaelekeza kutuma pesa kiasi cha shilingi 15,000/= kwenye namba ya simu 0685 794762 ili wapewe fulana na pia kupatiwa nafasi za kazi kwa vitendo katika Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka.
Hivyo, Wakala wa DART unapenda kutoa tamko rasmi kuwa hakuna utaratibu wowote unaohusu kuuza fulana wala nafasi za kazi kwa vitendo kwa wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali kama wanavyodai matapeli hao. Hivyo, kila atakayepata ujumbe huo ambao unasambaa kwenye mitandao ya kijamii anaombwa kupuuza.
Kutokana na utapeli huo Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka umechukua hatua ya kufikisha suala hilo kwenye mamlaka husika kwa ajili ya hatua zaidi.
Aidha, Wakala unatoa rai kwa wateja wake wote kuwa makini na matapeli wa aina hiyo.
Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zinazotolewa na Wakala wa DART, tafadhali tembelea tovuti (www.dart.go.tz) na kurasa za mitandao ya kijamii ya Facebook, X (Twitter), na Instagram@DARTMwendokasi au kupiga simu ya bure kwenye kituo chetu cha huduma kwa wateja kupitia namba 0800 110 147.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka- DART
Julai 25, 2024