Matukio

Habari

Waziri ataka Taa  zitumike kuongoza Mabasi Yaendayo Haraka

Waziri ataka Taa zitumike kuongoza Mabasi Yaendayo Haraka

Waziri wa nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Selemani Jafo hivi karibuni alimuagiza Mtendaji Mkuu wa DART, Mhandisi Ronald Lwakatare awasiliane na askari wa usalama wa barabarani kutafuta uwezekano wa kuruhusu taa za barabarani kwenye makutano yote ya barabara badala ya kutumia askari wa usalama wa barabarani kuongoza magari katika makutano hayo kwenye mfumo wa DART.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni muheshimiwa Jafo alisema kuwa kuongoza mtiririko wa magari katika makutano ya barabara kwa kutumia polisi wa usalama wa barabarani badala ya kutumia taa za barabarani husababisha ucheleweshaji wa mabasi ya DART kwenye makutano na vituo vingine.

Amesema watu wengi hivi sasa wamekuwa wakilalamika kuhusu mabasi ya DART kuchelewa kufika kwenye vituo vingi kutokana na msongamano wa magari unaosababishwa na askari wa usalama wa barabarani.

Waziri aliyetembelea Morocco na Kivukoni amesisitiza matumizi ya taa za barabarani ili kutimiza malengo ya mradi wa DART. Vilevile amelaumu utaratibu wa kutumia mabasi ya express yanayosafiri kutoka Kivukoni mpaka Kimara bila kusimama kwenye vituo vya kati na hivyo kuwaacha abiria wakiwa wamesongamana vituoni.

Katika mkutano huo wa waandishi wa habari waziri amewaonya madereva wote katika usafiri mchanganyiko wasipite katika barabara zilizotengwa kwaajili ya mabasi ya BRT.

Amewapiga marufuku madereva wa bajaji na bodaboda kutotumia vibaya njia za watembea kwa miguu na njia za baiskeli kwenye mfumo wa DART.

Awamu ya kwanza ya mradi wa DART ilianza shughuli zake za mabasi yaendayo kwa haraka tarehe 10 Mei, 2016 chini ya mtoa huduma wa mpito.


Ramani

    Hakuna Taarifa kwa sasa